Mr Fly Away
MR FLY AWAY / GREENE ERICK / DAR ES SALAAM

Kuna njia ya kutoka. Kazi yangu ni kukuonyesha ipi ni yako.

Kusoma, kufanya kazi, au kuishi nje ya nchi — njia ni nyingi na zinabadilika kila mwaka. Ninazifuatilia, nazihakiki, na nakuandikia kwa lugha unayoielewa.

Bila malipo Bila kunifuata kwanza Bila barua pepe
Bodi ya safari Hali ya sasa
DAR  →
Visa ya mwanafunzi F-1
Mwongozo tayari
DAR  →
CHINA Udhamini wa masomo
Inaandikwa
TZ   →
PASSPORT Maombi hatua kwa hatua
Inaandikwa
DAR  →
UTURUKI Masomo na ajira
Inakuja
DAR  →
KANADA Masomo na ukaazi
Inakuja
Wanafunzi
50+
Kituo
DAR TZ
Lugha
SW / EN
Miongozo
BURE
Nani mimi

Mr Fly Away ni mtu mmoja, si kampuni

Greene Erick — Mr Fly Away, Dar es Salaam
Greene Erick — ofisini, Dar es Salaam

Nimewasaidia zaidi ya wanafunzi 50 kutoka Tanzania kwenda kusoma nje ya nchi — kupitia kazi yangu ya kila siku katika sekta hii.

Nilianzisha Mr Fly Away kwa sababu moja: nimeona watu wengi mno wakidanganywa. Wanalipa pesa nyingi kwa taarifa ambazo serikali huchapisha bure. Wananunua nyaraka za uongo kutoka kwa watu wanaowaita "wataalamu". Wanaambiwa visa imehakikishwa — kisha wanakataliwa na kupoteza kila kitu.

Kwa hiyo miongozo yangu ni bure, na nimeandika wazi vitu ambavyo siwezi kukuahidi. Ukiamua kunilipa, ni kwa msaada wa kesi yako mwenyewe — si kwa taarifa ambazo tayari ni haki yako.

Greene Erick Mr Fly Away · Dar es Salaam
Kanuni

Vitu vitatu ambavyo sitakuahidi kamwe

Hizi si maneno ya kujitetea. Ni jinsi ya kumtambua tapeli — hata kama ana ofisi nzuri, simu inayopokelewa, na wateja wanaomsifu.

01

Siwezi kukuhakikishia visa

Hakuna mtu anayeweza. Uamuzi uko mikononi mwa afisa wa ubalozi peke yake. Yeyote anayekuahidi visa anakudanganya, na anajua anakudanganya.

02

Sitakuuzia nyaraka

Hakuna bank statement ya kununua, hakuna barua ya uongo. Hati za uongo husababisha kukataliwa milele — si 214(b) inayoweza kurekebishwa.

03

Sina njia ya mkato

Hakuna mtu wa ndani, hakuna njia ya siri, hakuna "connection". Kilichopo ni maandalizi mazuri, nyaraka za kweli, na maombi ya uaminifu.

Ninachojenga

Mwongozo mmoja kwa kila njia — mmoja baada ya mwingine

Kila mwongozo huchukua wiki kadhaa kwa sababu kila ada, tarehe na sheria huhakikiwa kwenye tovuti rasmi kabla ya kuchapishwa. Ni polepole kwa makusudi.

DAR → USAVisa

Visa ya Mwanafunzi ya Marekani (F-1)

Vitu 5, ada zote, sheria nne mpya za 2026, maswali 9 ya interview. Kurasa 13.

Tayari
DAR → CHINAUdhamini

Udhamini wa masomo China

Jinsi ya kuomba, gharama halisi kwa mwaka, na tarehe za madirisha.

Inaandikwa
TZ → PASSPORTNyaraka

Passport ya Tanzania

Hatua kwa hatua, nyaraka zinazohitajika, gharama, na muda halisi.

Inaandikwa
DAR → UTURUKIMasomo

Masomo na ajira Uturuki

Njia inayokua kwa kasi kwa Watanzania. Mwongozo unafuata.

Inakuja
DAR → WORLDKazi

Kufanya kazi nje ya nchi

Njia halali za ajira na jinsi ya kutambua matangazo ya uongo.

Inakuja

Unataka njia fulani ipewe kipaumbele? Niandikie neno NJIA na jina la nchi. Ninazoulizwa zaidi ndizo ninazoandika kwanza.

Fursa

Jiandae kabla dirisha halijafunguka

Udhamini huja na kuondoka haraka. Wanaofanikiwa si wenye bahati — ni waliokuwa na passport, vyeti na bank statement tayari siku dirisha lilipofunguka.

Kwa sasa hakuna dirisha lililo wazi. Niandikie neno FURSA na nitakujulisha lijalo likifunguka — pamoja na orodha ya nyaraka za kuandaa mapema, ili usikimbie siku ya mwisho.

Niongeze kwenye orodha
Niulize