Kusoma, kufanya kazi, au kuishi nje ya nchi — njia ni nyingi na zinabadilika kila mwaka. Ninazifuatilia, nazihakiki, na nakuandikia kwa lugha unayoielewa.
Nimewasaidia zaidi ya wanafunzi 50 kutoka Tanzania kwenda kusoma nje ya nchi — kupitia kazi yangu ya kila siku katika sekta hii.
Nilianzisha Mr Fly Away kwa sababu moja: nimeona watu wengi mno wakidanganywa. Wanalipa pesa nyingi kwa taarifa ambazo serikali huchapisha bure. Wananunua nyaraka za uongo kutoka kwa watu wanaowaita "wataalamu". Wanaambiwa visa imehakikishwa — kisha wanakataliwa na kupoteza kila kitu.
Kwa hiyo miongozo yangu ni bure, na nimeandika wazi vitu ambavyo siwezi kukuahidi. Ukiamua kunilipa, ni kwa msaada wa kesi yako mwenyewe — si kwa taarifa ambazo tayari ni haki yako.
Hizi si maneno ya kujitetea. Ni jinsi ya kumtambua tapeli — hata kama ana ofisi nzuri, simu inayopokelewa, na wateja wanaomsifu.
Hakuna mtu anayeweza. Uamuzi uko mikononi mwa afisa wa ubalozi peke yake. Yeyote anayekuahidi visa anakudanganya, na anajua anakudanganya.
Hakuna bank statement ya kununua, hakuna barua ya uongo. Hati za uongo husababisha kukataliwa milele — si 214(b) inayoweza kurekebishwa.
Hakuna mtu wa ndani, hakuna njia ya siri, hakuna "connection". Kilichopo ni maandalizi mazuri, nyaraka za kweli, na maombi ya uaminifu.
Kila mwongozo huchukua wiki kadhaa kwa sababu kila ada, tarehe na sheria huhakikiwa kwenye tovuti rasmi kabla ya kuchapishwa. Ni polepole kwa makusudi.
Vitu 5, ada zote, sheria nne mpya za 2026, maswali 9 ya interview. Kurasa 13.
Jinsi ya kuomba, gharama halisi kwa mwaka, na tarehe za madirisha.
Hatua kwa hatua, nyaraka zinazohitajika, gharama, na muda halisi.
Njia inayokua kwa kasi kwa Watanzania. Mwongozo unafuata.
Njia halali za ajira na jinsi ya kutambua matangazo ya uongo.
Unataka njia fulani ipewe kipaumbele? Niandikie neno NJIA na jina la nchi. Ninazoulizwa zaidi ndizo ninazoandika kwanza.
Udhamini huja na kuondoka haraka. Wanaofanikiwa si wenye bahati — ni waliokuwa na passport, vyeti na bank statement tayari siku dirisha lilipofunguka.
Kwa sasa hakuna dirisha lililo wazi. Niandikie neno FURSA na nitakujulisha lijalo likifunguka — pamoja na orodha ya nyaraka za kuandaa mapema, ili usikimbie siku ya mwisho.